Ingia / Jisajili

Wakristu Tulijenge Kanisa

Mtunzi: Dr.vasco A Kapinga
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr.vasco A Kapinga

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Vasco Aidan

Umepakuliwa mara 457 | Umetazamwa mara 1,483

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

Wakristu tuamke tulijenge kanisa kwani ndio ni wa misionari*2 amka amka wewe uliyesahau kanisa linahitaji zaka yako,nasadaka na michango mbalimbali kanisa la Mungu lakutegemea,( ha ha ha ha hakuna wazungu hakuna Wahindi hakuna Wachina hakuna wakulijenga kanisa hakuna)*2

Mashairi

1. Tuziache dhana zile za zamani,wazungu ndio kanisa kudumisha,

Wazungu Wahindi walisha enda kwao,hawapo tena, sasa ni wenyewe tujifunge mikanda, tusonge mbele.

2. Tujitolee kwa moyo kwa bidii,kwa hali mali na muda tujitoe,
tusingoje kusukumwa na viongozi,tuna watesa,
tujitoe kwahiari kutimiza wajibu wetu.
3. Ithaminishe kazi yako na ya Mungu,ipi ni yako na ipi ni ya Mungu
ni wazi ni Mungu kakujalia hiyo,yote ni yake
chukua muda umtumikie kulijenga kanisa lake.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa