Mtunzi: Thomas P. Bingi
> Mfahamu Zaidi Thomas P. Bingi
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas P. Bingi
Makundi Nyimbo: Juma Kuu
Umepakiwa na: Thomas Bingi
Umepakuliwa mara 500 | Umetazamwa mara 1,819
Download Nota Download MidiYesu akamwambia Simoni nifanyalo wewe hujui hujui sasa, lakini utalifahamu utalifahamu baadae.
Mashairi
1.Yesu aliondoka chakulani akaweka kando mavazi yake
Akatwaa kitambaa akajifunga kiuno-ni.
2.Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi miguu
Na kuwafuta kwa kile kitambaa alichojifu-nga.
3.Wafalme wa Dunia hutawala,Na wenye mamlaka juu yao huitwa wenye fadhili,
Lakini kwenu ninyi sivyo, Bali aliye mkubwa kati yenu, na awe kama aliye mdo-go.
4.Nami nawawekea ninyi ufalme,kama vile baba yangu alivyo niwekea mimi,
Ili mpate kula, na kunywa mezani pangu katika ufalme wa-ngu.