Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 3,925 | Umetazamwa mara 10,411
Download Nota Download MidiKIITIKIO
Ni Mungu wetu Bwana wetu atukuzwe popote kaumba nyimbo na sauti aimbiwe na wote ndiye Bwana Amen wa Ma Bwana Aleluya ni Mungu Amen wa miungu Aleluya
Amen Aleluya Aleluya Amen Aleluya Aleluya
1. Mbingu ni juu ndiko anakaa akitukuzwa na malaika
Aliziumba mbingu na dunia akazifanya hivi
2. Alikataza asiabudiwe awa yeyote zaidi yake
Ana stahili kwani peke yake aliyaweka yote
3. Akamtoa mwanaye pekee aning’inizwe tuwe salama
Upendo gani haueleweki haupimiki kamwe
4. Aliyesema niite daima niite nami nitaitika
Nitalifanya jambo juu yako nitalifanya upya