Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: Stanslaus Butungo
Umepakuliwa mara 2,452 | Umetazamwa mara 6,430
Download Nota Download MidiKiitikio:
Alidharauliwa na kukataliwa na watu mtu wa huzuni nyingi, mtu wa huzuni nyingi mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko X2
Mashairi:
1. Na kila mtu ambaye watu humficha nyuso zao, alidharauliwa na hatukumuhesabu kitu, hakika ameyachukua masikitiko yetu kajivika huzuni zetu
2. Lakini tulimdhania ya kuwa yeye amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuumizwa sanana kuchubuliwa vibaya, adhabu ya-dhambi zetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepone.
3. Alionewa lakini alinyenyekea wala hakukifungua kinywa chake kama kondoo apelekwaye machinjoni kama kondoo anyamazavyo wakakata manyoya yake
4. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya, pamoja na matajiri katika kufa kwakeingawa hakutenda jeuri wala hapakuwa na hila kinywani mwake.