Ingia / Jisajili

Baba Ninawaombea Hawa

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Kupaa kwa Bwana

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 1,994 | Umetazamwa mara 5,961

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

BABA NINAWAOMBEA HAWA. Yoh 17: 11, 15-17, 21-23

Baba ninawaombea hawa ulionipa wawe kitu kimoja kama tulivyo wamoja x2. Nimewapa utukufu, ule ulionipa mimi, ili ulimwengu uwatambue kama wanafunzi wangu x2

  1. Baba Mtakati-fu kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa wawe na umoja kama tulivyo na umoja
  2. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni nami vivyo hivyo ninawatuma ulimwenguni
  3. Mimi siombo kwamba uwatoe katika ulimwengu bali uwalinde na yule mwovu na yule mwovu
  4. Wao si wa ulimwengu kama nisivyo wa ulimwengu uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndilo kweli, neno lako ndilo kweli ndilo kweli Ee Bwana


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa