Ingia / Jisajili

Uusitiri Uso Wako Mungu

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma | Mazishi | Zaburi

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 836 | Umetazamwa mara 3,162

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

UUSITIRI USO WAKO MUNGU  Zab 32:5, 38:4-5, 39:4-5, 51:9-11

Ee Mungu Uusitiri uso wako, ufiche uso wako kwa mikono yako, usitazame dhambi nilizozitenda, uzifute dhambi zangux 2

  1. Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu, nalisema nitayakiri maasi yangu, nawe ukanisamehe upotovu wangu
  2. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kama mzigo mzito zimenielemea, jeraha zangu zimenuka zimeoza, kwa ajili ya upumbavu upumbavu wangu
  3. Bwana unijulishe mwisho wangu, na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani, nijue jinsi nilivyo dhaifu mbele zako, maisha yangu si kitu mbele zako
  4. Ee Mungu uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako, wala Roho wako usiniondolee

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa