Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 1,914 | Umetazamwa mara 5,252
Download Nota Download MidiASANTE MUNGU, ASANTE – F. KITUYI
Kiitikio:
Asante Mungu asante, ninakushukuru;
Asante kwa mema yote, Mungu Baba asante. x2
Asante Mungu asante, asante Mungu asante,
Kwa mema unayonipa, Mungu Baba asante. x2
1. Kwa uzima wangu na uhai wangu,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
Kwa chakula changu na kinywaji changu,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
2. Kwa mapato yangu, mahitaji yangu,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
Kwa wazazi wangu, na watoto wangu,
Uumenipa bure, Mungu Baba asnte.
3. Kwa masomo yangu, na elimu yangu,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
Kwa walimu wangu, wahadhiri wangu,
Uumenipa bure, Mungu Baba asante.
4. Kwa askofu wangu, na mapadre wangu,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
Na watawa wote, watumishi wako,
Umenipa bure, Mungu Baba asante.
5. Na matendo yako, maajabu kweli,
Wewe Mungu wangu, Mungu Baba mwumba.
Na nitakusifu, nitakushukuru,
Daima milele, na milele, Amina.