Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi
Makundi Nyimbo: Mwanzo
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 3,013 | Umetazamwa mara 7,135
Download Nota Download MidiNJONI NYOTE NYUMBANI – F. B. KITUYI
Kiitikio:
Njoni nyote nyumbani mwake,
Njoni tumwabudu Mwenyezi Mungu,
Tumtolee sadaka safi, njoni tukamwabudu. x2
1. Tuingie nyumba ya Bwana tukatubu dhambi zetu;
Tuwe safi mbele za Bwana, tumwabudu Mwenyezi Mungu.
2. Ndiye Mungu mwumba wetu, tumshukuru tumwombe;
Mahitaji ya kila siku, tumwabudu Mwenyezi Mungu.
3. Tumwimbie nyimbo za shangwe, tujongee mbele zake;
Furahini viumbe wote, tumwabudu Mwenyezi Mungu.
4. Cheza ngoma pia kayamba, tumpigie na vinanda;
Tukapige vigelegele, tumwabudu Mwenyezi Mungu.