Mtunzi: Wolford P. Pisa (WPP)
> Mfahamu Zaidi Wolford P. Pisa (WPP)
> Tazama Nyimbo nyingine za Wolford P. Pisa (WPP)
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Wolford Peter Pisa
Umepakuliwa mara 503 | Umetazamwa mara 1,944
Download Nota Download MidiBASI JIWEKENI
Chorus; Basi basi jiwekeni chini ya Mungu, mpingeni shetani, naye atawakimbia atawakimbia x2
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia, naye atawakaribia karibia ninyi x2
Mashairi; 1. Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? si humu, katika tamaa
zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu.
2. Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya
vita na kupigana, wala hmna kitu kwa kuwa hamwombi.
3. Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
4. Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila
atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.