Ingia / Jisajili

Bwana Ni Mchunga Wangu

Mtunzi: Wamalwa Wanyama
> Tazama Nyimbo nyingine za Wamalwa Wanyama

Makundi Nyimbo:

Umepakiwa na: Silvanos Wamalwa

Umepakuliwa mara 597 | Umetazamwa mara 2,222

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Bwana ni mchunga wangu sitapungukiwa na kitu, sitahitaji chochote maana ananijalia

S/T: Katika malisho malisho ... majani mabichi, Bwana huwa ananilaza ananilaza

A/B: ...malisho ya majani (A: mabichi) majani mabichi ... huwa ananilaza, ananilaza

S/T: Kando ya maji matulivu ... maji matulivu, Yeye huniongoza mimi, huniongoza

A/B: ... ya maji (yaliyo) matulivu maji matulivu ... huniongoza mimi, huniongoza

  1. Hunihuisha nafsi na kuniongoza katika haki, Chini ya mbawa zake napata kimbilio siku zote.
  2. Yupo pamoja nami, gongo lake na fimbo vyanifariji, ananiandalia karamu mbele ya watesi wangu.
  3. Palipo na mashaka ayatimua yanaondoka, moyoni ni amani, tulizo kama usingizi mnono.
  4. Bwana ni mchunga wangu sitapungukiwa hata milele, Bwana ni mchunga wangu sitapungukiwa hata milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa