Mtunzi: Wilhelm A. Kiwango (W. Kiwango)
> Mfahamu Zaidi Wilhelm A. Kiwango (W. Kiwango)
> Tazama Nyimbo nyingine za Wilhelm A. Kiwango (W. Kiwango)
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Willy Kiwango
Umepakuliwa mara 1,951 | Umetazamwa mara 6,046
Download Nota Download MidiKiitikio:
Aleluya Aleluya Bwana Yesu kweli amefufuka x2 Kafufuka mzima kafufuka alivyosema! Aleluya aleluya Bwana Yesu Kweli amefufuka
Viimbilizi
1. Mwokozi wetu kafufuka, ametoka kweli ni mzima, njoni wote tumshangilie twimbe wote aleluya
2. Kaburi kaliacha wazi, ametoka yukiwa mzima, wale walinzi wote wamelala kwani Bwana Mungu halindwi
3.Ametutoa utumwani, utumwani mwa mwovu shetani, minyororo yake kaikata nasi tumekuwa huru
4.Na sisi sote tumekuwa, tumekuwa watoto wa Mwanga, Kristo ametutoa gizani njoni wote tumshangilie.