Maneno ya wimbo
CHAKULA TOKA MBINGUNI
INTRO: Aulaye mwili wangu na Kuinywa damau yangu , anauzima wa milele asema
Bwana. CHORUS: Hiki ni Chakula ( kweli) kutoka Mbinguni (yeye) alaye chackula (hiki)
hatakufa x2. Tule mwili wake Kristu tunywe damu yake, tupate uzima wa
milele
STANZAS:
1a. Tumealikwa kwa karamu yake Bwana, karamu ya upendo wake Bwana Yesu
1b. Ni mwili wake kwa maumbo ya mkate, ni damu yake kwa maumbo ya divai
2a. Moyoni mwetu uingie uitakase, uishibishe nafsi yetu tuwe safi, 2b. Wewe ni Bwana wetu pia Mungu wetu, upendo wako kwetu sisi ni ya kweli
3a. Ee mkate safi wa uzima twakusifu, we wastahili sifa pia na heshima. 3b. We ekaristi ndio fumbo takatifu, ndio chakula bora cha wokovu wetu.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu