Mtunzi: Peter.g.lulenga
> Mfahamu Zaidi Peter.g.lulenga
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter.g.lulenga
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Geophrey Lulenga
Umepakuliwa mara 514 | Umetazamwa mara 2,196
Download NotaEE BWANA NITAKUIMBIA ZABURI
KIITIKIO:Ee Bwana,Ee Bwana, Ee Bwana, Ee Bwana mbele ya miungu nitakuimbia zaburi.
MASHAIRI
1.Nitakushukuru kwa moyo wangu wote mbele ya miungu nitakuimbia zaburi, nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, nitalishukuru jina lako.
2.Nitalishukuru jina lako kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, kwa maana umeikuza ahadi kuliko jina lako lote, siku ile niliyokuita uliniitikia.
3.Ee Bwana wafalme wote wa dunia watakushukuru watakapoyasikia maneno ya kinywa chako, naam wataziimba njia za Bwana, kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.
4.Na mkono wako wa kuume utaniokoa, Bwana utanitimilizia mambo yangu, Ee Bwana fadhili zako ni za milele uziache uziache uziache kazi za mikono yako.