Mtunzi: Emil E Muganyizi
> Tazama Nyimbo nyingine za Emil E Muganyizi
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Emil Mwemezi
Umepakuliwa mara 1,629 | Umetazamwa mara 3,933
Download Nota Download MidiEe Mungu wangu Mfalme (Mfalme) nitakutukuza nitalihimidi jina lako milele na milele X2
01. Bwana ana fadhili ni mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa rehema, Bwana ni mwema kwa watu wote na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
02. Bwana kazi zako zote zitakushukuru, na wacha Mungu wako watakuhimidi, wataunena utukufu wa Ufalme wako na kuuhadithia uweza wako.
03. Ili kuwajulisha matendo yake makuu, na utukufu wa fahari ya ufalme wake, Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.