Ingia / Jisajili

Fahari ya ukatoliki

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 823 | Umetazamwa mara 2,677

Download Nota
Maneno ya wimbo

(Ninasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi, Ninaungama ubatizo mmoja. Ninasadiki kwa Roho Mtakatifu, Nakanisa Katoliki la Mitume; Niliapa mwenyewe siku ya ubatizo wangu, kwamba nitaishika Dini yangu siikani; Ninaona fahari kuitwa mkatoliki x2)

1.Kanisa takatifu Katoliki la Mitume limejengwa chini ya mwamba thabiti, msingi wake u juu ya mlima mtakatifu hautikisiki halitaanguka na halitatikisika.

2.Kanisa takatifu Katoliki la Mitume twaukiri Utatu Mtakatifu yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu naona fahari kuitwa Mkatoliki.

3.Kanisa takatifu Katoliki la Mitume limejaa miujiza ya Mungu kweli , imani thabiti iliyowekwa na Yesu juu ya Mitume kamwe sitayumbishwa na manabii wa uongo.

4.Kanisa takatifu Katoliki la Mitume tunaona fahari ya msalaba, Msalaba wa Yesu ambapo Wokovu wa Dunia umetundikwa ndiyo maana twapiga ishara ya masalaba.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa