Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 595 | Umetazamwa mara 1,803
Download Nota Download MidiYesu wangu, nakushukuru, kwa kunilisha mwili wako. umininywesha damu yako nashukuru x2. {chakula chako kinanishibisha, na damu yako, huniburudisha, milele milele milele, milele, milele milele nashukuru x2}
1.Nikiwa na Njaa, unanilisha ae Bwana, nashukuru. Nikiwa na kiu unaninywesha, ae Bwana, nashukuru. Ajali magonjwa, waniepusha ae Bwana, Nashukuru.
2.Ingia moyoni unishibishe; ae Bwana nashukuru. Wewe ni rafiki na kiongozi; ae Bwana, nashukuru. Nijaze upendo na ukarimu; ae Bwana nashukuru.
3.Katika huzuni wanifariji; ae Bwana nashukuru. Mitego ya mwovu waniepusha; ae Bwana, nashukuru. Nielemewapo waniinua; ae Bwana, nashukuru.
4.Nyakati za vita unanilinda; ae Bwana, nashukuru. Chakula chanipa uzima mpya; ae Bwana nashukuru. Umenishibisha umeninywesha; ae Bwana nashukuru.