Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Richard Samson
Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 19 Mwaka C
Heri taifa ambalo Bwana, Ambalo Bwana ni Mungu wao x2.
1. Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
2. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojea fadhili zake. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa.
3. Nafsi zetu zinamngoja Bwana, Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi, Kama vile tulivyokungoja Wewe.