Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,599 | Umetazamwa mara 4,456
Download NotaNi nani mnayemtafuta? Ni Yesu ni Yesu Mnazareti x 2
Yesu akajibu akawaambia akawaambia makutano Ni Mimi ni Mimi ni Mimi mnayemtafuta x2
Nao makutano waliposikia hivyo wakaanguka wakaanguka chini mara Yesu akawauliza tena mwamtafuta nani?
Nao wakajibu twamtafuta Yesu twamtafuta Yesu, Yesu Mnazareti X 2
Yesu akajibu akawaambia nimekwisha waambia Ndiye mimi basi ikiwa ni mimi mnayemtafuta waacheni hawa waende zao
Naye Simoni Petro aliposikia hivyo akatoa upanga wake akatoa upanga wake akamkata sikio la kuume yule mtumwa wa kuhani mkuu akamkata sikio kwa upanga.
Basi Yesu akamwambia Petro: Hebu rudisha upanga wako alani mwake kwa maana imenipasa kukinywea kikombe hiki
Imenipasa (kweli) Imenipasa (kweli) Imenipasa kukinywea kikombe hiki x 2
Imenipasa kufa msalabani ili kuleta wokovu imenipasa kufa msalabani ili kuleta wokovu imenipasa kufa msalabani ili kuleta wokovu
Imenipasa (kweli) imenipasa (kweli) Imenipasa kukinywea kikombe hiki x 2