Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Gervas Kombo
Umepakuliwa mara 2,974 | Umetazamwa mara 7,445
Download Nota Download Midi1. Kina Baba pigeni makofi na kina mama vigelegele tuizungukeni meza tukapokee Ekaristi takatifu
Tuichumie maua mazuri tuipambe kwa mishumaa mingi tuizungukeni meza…
Karibuni makuhani kwa furaha sogea watawa wote wa kanisa njooni walei kwa shangwe vifijo na kwa kurukaruka tuizungukeni meza tukapokee Ekaristi takatifu
2. Furaha ndani ya nyoyo zetu, Baraka tutajaziwa tele, tuizungukeni.......
Ndani ya Yesu tutaingia, na Yesu ndani ya Roho zetu, tuizungukeni....
3. Vinyongo tuondoleaneni, tukapokee kwa moyo safi, tuizungukeni.......
Kununiana tusahau, twende kwenye karamu ya Bwana, tuizungukeni...
4. Wokovu tuutafute wapi, kama sii ndani ya Ekaristi, tuizungukeni......
Mungu mwenyewe ni huyu hapa ndani ya ngano na mzabibu, tuizungukeni....