Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mwanzo | Zaburi
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,964 | Umetazamwa mara 5,156
Download Nota Download MidiKiitikio:
Mawazo ninayowawazia ninyi ni mawazo ya amani, ni mawazo ya amani wala si mabaya(x2). Nanyi mtaniita nami nitawasikiliza, nami nitawarudisha kutoka mahali pote, watu wenu waliofungwa, watu waliofungwa.
Mashairi:
1. Nami nitawapa moyo, nami nitawapa moyo, wanijue ya kuwa mimi ni bwana, nao watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote
2.Mtafuteni bwana maadamu anapatikana, mwiteni maadamu yu karibu, mtu mbaya na aache hila zake na mtu asiye haki aache mawazo yake.
3.Ombeni nanyi mtapata, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa.