Ingia / Jisajili

MISA YA MT.KAROLI LWANGA(MASHAHIDI WA UGANDA)

Mtunzi: Peter.g.lulenga
> Mfahamu Zaidi Peter.g.lulenga
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter.g.lulenga

Makundi Nyimbo: Misa

Umepakiwa na: Geophrey Lulenga

Umepakuliwa mara 2,265 | Umetazamwa mara 5,645

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

                                                                                                        MISA YA MT.KAROLI LWANGA

                                                                                                       1. BWANA UTUHURUMIE(KYRIE)

Bwana utuhurumie,Bwana utuhurumie x 2,(Kristo) utuhurumie kristo utuhurumie x2,Bwana utuhurumie,Bwana utuhurumie x2

                                                                                                                2.UTUKUFU(GLORIA)

Utukufu kwa Mungu juu na amani duniani kwa watu aliowaridhia.Tunakusifu, tunakuheshimu tunakuabudu,tunakutukuza.Tunakushukuru kwa ajili ya utukufu,utukufu wako mkuu,ee Bwana Mungu mfalme wa mbinguni ,Mungu Baba mwenyezi.Ee Bwana Yesu kristo mwana wa pekee,ee Bwana Mungu mwanakondoo wa Mungu,mwana wa Baba.Mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu utuhurumie,ewe mwenye kuondoa dhambi za ulimwengu,pokea ombi letu,ewe mwenye kuketi kuume kwa baba utuhurumie.Kwa kuwa ndiwe uliye peke yako mtakatifu,peke yako Bwana uliye juu kabisa,uliye juu,Yesu kristo.Pamoja na roho mtakatifu katika utukufu wa Mungu baba,AMINA.

                                                                                                              3.MTAKATIFU(SANCTUS)

Mtakatifu mtakatifu Bwana,mtakatifu Bwana Mungu wa majeshi x2.Mbingu na ulimwengu zimejaa utukufu wako,zimejaa utukufu wako x2.

Hosana (hosana) hosana (hosana) hosana juu mbinguni x2.Mbarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana,kwa jina la Bwana hosana juu mbinguni.(Baada ya kuimba mbarikiwa tuimbe hosana tena mara mbili).

                                                                                                              4.MWANAKONDOO(AGNUSDEI)

Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu, utuhurumie x2.Mwanakondoo wa Mungu uondoaye dhambi za ulimwengu,utujalie amani.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa