Ingia / Jisajili

MPENI KAISARI

Mtunzi: Obuya Joseph Ochieng
> Mfahamu Zaidi Obuya Joseph Ochieng
> Tazama Nyimbo nyingine za Obuya Joseph Ochieng

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: OBUYA JOSEPH

Umepakuliwa mara 819 | Umetazamwa mara 1,987

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
MPENI KAISARI 1a. Hebu jiulize, maarifa hata nguvu ya kufanya kazi , yametoka wapi, kwa hakika yametoka kwa Mungu 1b. Fedha na dhahabu, nyumba nzuri nguo zako na magari zako , yametoka wapi kwa hakika yametoka kwa Mungu Kiitikio: Mpeni, Kaisari yalo' yake, pia mpeni Mungu, yaliyo yake yaliyo yake Mungu 2a. Hebu jiulize, pesa zako na hazina zako kwenye benki ,yametoka wapi, kwa hakika yametoka kwa Mungu 2b. Hata na mifugo, na nimea nanafaka zako kwenye ghala, yametoka wapi, kwa hakika yametoka kwa Mungu 3a. Hebu jiulize, na hekima na talanta hata ubunifu, yametoka wapi , kwa hakika yametoka kwa Mungu 3b. Jua na mvua, na bahari na misitu na rasilmali ,yametoka wapi ,kwa hakika yametoka kwa Mungu 4a. Hebu jiulize, kitu gani utampa Mungu muumba wako, kwa kumshukuru, kwa hakika Mungu anakupenda 4b. Hakuna zawad,i utampa Mungu wako wa kumfidia, kuliko kusali, na kufuata maagizo ya Mungu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa