Ingia / Jisajili

Mpigie Mungu Kelele

Mtunzi: John Mgandu
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mgandu

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 17,171 | Umetazamwa mara 27,118

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mpigie Mungu kelele za shangwe nchi yote Imbeni, imbeni, imbeni, imbeni utukufu (wa jina lake) tukuzeni, tukuzeni sifa zake tukuzeni sifa zake sifa zake.

  1. Mwambieni Mungu mwambieni matendo yako yanatisha, yanatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
     
  2. Nchi yote nchi yote, itakusujudia na kukuimbia, itakusujudia na kukuimbia naam italiimbia jina lako jina lako.
     
  3. Njoni njoni njoni yatazameni matendo matendo ya Mungu, hutisha hutisha hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu wanadamu.

Maoni - Toa Maoni

REMIJO SANGA Nov 09, 2017
Wimbo mzuri mungu Wa mbinguni akubariki sana

Toa Maoni yako hapa