Ingia / Jisajili

Mshukuruni Bwana

Mtunzi: John Mgandu
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mgandu

Makundi Nyimbo: Pasaka | Shukrani

Umepakiwa na: Beatus Idama

Umepakuliwa mara 9,593 | Umetazamwa mara 18,915

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake, ni za milele x 2

  1. Washukao baharini, katika merikebu, wafanyao kazi yao katika maji mengi hao huziona kazi za Bwana, na maajabu yake vilindini.

  2. Maana husema, akavumisha upepo na dhoruba, ukayainua juu mawimbi yake wapanda mbinguni wateremka vilindini, nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya.

  3. Wakamlilia Bwana, wakamlilia katika dhiki zao, akawaponya na shida zao tuliza dhoruba ikawa shwari, mawimbi yake, yakanyamaza.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa