Mtunzi: Wolford P. Pisa (WPP)
> Mfahamu Zaidi Wolford P. Pisa (WPP)
> Tazama Nyimbo nyingine za Wolford P. Pisa (WPP)
Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Wolford Peter Pisa
Umepakuliwa mara 1,755 | Umetazamwa mara 5,186
Download Nota Download MidiKiitikio:
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema mwema(mwema) kwa maana fadhili zake ni za milele, kwa maana fadhili zake ni za milele. Mashairi
1. Washukao baharini katika merikebu, wafanyao kazi zao katika maji mengi hao huziona kazi za Bwana, na maajabu yake, na maajabu yake, na maajabu yake vilindini.
2. Kwa maana husema kavumisha upepo na dhoruba, ukayainua juu mawimbi yake wapanda mbinguni wateremka vilindini, nafsi yao yayeyuka, nafsi yao yayeyuka, nafsi yao yayeyuka kwa hali mbaya.
3.Wakamlilia Bwana, katika dhiki zao akawaponya na shida zao hutuliza dhoruba ikawa shwari, nayo mawimbi yake, nayo mawimbi yake, nayo mawimbi yake yakanyamaza.