Mtunzi: Peter Makolo
> Mfahamu Zaidi Peter Makolo
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter Makolo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Peter Makolo
Umepakuliwa mara 687 | Umetazamwa mara 2,806
Download Nota Download Midi1a) Ninakutazama Yesu wangu, (Mwokozi), U Mungu wangu nakuamini pokea ombi langu.
2b)Ninakuhitaji Yesu wangu, (Mwokozi), Huisha moyo wangu dhaifu pokea ombi langu.
Kiitikio:
{(I&III) Kwa Imani kuu} nakuona Bwana, ninakuamini Mungu wangu, (Mwokozi), naamini
{II&IV(Kwa Imani)} nakuona Bwana, ninakuamini Mungu wangu, (Mwokozi), naamini
utanishindia×2
2a) Katika safari ya Imani, (ni nzito), mawimbi ma-kali yanisonga, hima nisaidie.
2b) Kuishinda dhambi ninataka, (mwanao), mwili u dhaifu naanguka, hima nisaidie.
3a)Taabu na shida za duni-a, (zazidi), zinanielemea mwanao, uniokoe Bwana.
3b)Unishike mkono Yesu wa-ngu, (Mwokozi), uniongoze kwa neno lako, uniokoe Bwana.
4a) Ninajipa moyo Yesu wangu, (Mwokozi), ulinifi-a m salabani kwa kunipenda sana.
4b)Ninajikabidhi kwako Yesu, (Mwokozi), ninakutazama kwa imani pokea ombi langu.
Kimalizio:
Nakutazama kwa Imani×6