Ingia / Jisajili

Ungana Nami Leo

Mtunzi: Peter Makolo
> Mfahamu Zaidi Peter Makolo
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter Makolo

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: Peter Makolo

Umepakuliwa mara 502 | Umetazamwa mara 2,054

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

 1. Mpenzi wangu ungana nami  leo,
  Kwa heshima kubwa na kwa unyenyekevu
  Twende kwake Mungu akabariki pendo letu.
  Ili tuanze maisha yetu tukiwa naye.

 2. Mungu Mwenyezi ametuita leo,
  Tuanze ndoa yetu kwa maongozi yake,
  Twende tukaishi kwa upendo na kwa amani.
  Tumtumikie Mungu wetu kiaminifu.
   
 3. Sala ziwe msingi wa ndoa yetu,
  Tuvumiliane tunapokoseana,
  Kwa imani kuu tumtazame Yesu Kristu.
  Tukishikamana naye atatushindia.
   
 4. Mungu mwenye enzi ututazame sisi,
  Tuongoze wanao kwa hekima yako,
  Tushikamane na kusaidiana siku zote.
  Kwa hekima yetu hatuwezi tutashindwa.
   
 5. Mungu Baba Mwana na Roho Mtakatifu,
  Twajikabidhi kwako wanao leo,
  tujalie tuishi kiaminifu
  Tuwe mfano mwema kwa taifa lako.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa