Mtunzi: Joseph Nyarobi
> Mfahamu Zaidi Joseph Nyarobi
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Nyarobi
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Joseph Nyarobi
Umepakuliwa mara 1,937 | Umetazamwa mara 4,315
Download Nota Download MidiUTANGULIZI
Leo ni siku ya furaha, siku takatifu tuliyoingoja, siku ya kuzaliwa mwokozi wetu. Yerusalemu ni furaha, shangwe zimetanda wengi wakiimba, noeli Krismasi bwana kazaliwa.
KIITIKIO
Nifuraha kote duniani, mkombozi wetu kazaliwa, Yerusalemu yatetema kwa, furaha kumlaki Bwana, tupaze sauti tukisema, Aleluya Bwana kazaliwa, kwa ajili yetu amezaliwa mtoto mwenye uweza wa kifalme
1. Ni Bethlehemu pangoni Bwana Yesu amezaliwa (ba-si) twendeni wote twendeni, tukamsujudie
2. leo usiku wa manane Bwana Yesu amezaliwa,(wo-te) twendeni wote twendeni, tukamsujudie
3.Jina lake Emanueli yaani Mungu pamoja nasi (wo-te) twendeni wote twendeni, tukamsujudie
4. Ni mfalme wa wafalme ni mkuu wa wakuu (wo-te), twendeni wote twendeni, tukamsujudie
KIBWAGIZO
Aleluya Aleluya, tufurahi sote, kwani mwana wa Mungu leo amezaliwa, ni mkuu wa wakuu, mfalme wa wafalme ni (Masihi) ndiye mwana wa Mungu leo amezaliwa.