Ingia / Jisajili

Nikushukuruje Mungu Wangu

Mtunzi: Alex Rwelamira
> Mfahamu Zaidi Alex Rwelamira
> Tazama Nyimbo nyingine za Alex Rwelamira

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Alex Rwelamira

Umepakuliwa mara 449 | Umetazamwa mara 799

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Nikushukuruje Mungu wangu kwa uliyonitendea (Bwana) mimi kiumbe wako niliye mdogo (sana) mbele yako X2

Umeniumba mimi (Bwana) ukanipa uhai umenilinda siku zote ukanikinga na maradhi

Umenipa familia (bora) umenipa marafiki (wengi) umenipa nao umri (mrefu) nikulipe nini Bwana (wewe) umenitendea mema mengi mimi nasema asante (sana) Mungu wangu X2

1. Nitakushukuru Bwana katika kusanyiko kubwa nitakusifu kati ya watu wengi kwa baraka zote na neema nyingi unazonikirimia pasipo mastahili yangu wewe umenitunza nina afya ya mwili na roho

2. Nitayainua macho yangu niitazame milima msaada wangu u katika Bwana aliyezifanya mbingu na nchi yeye ndiye Mungu wangu amenivusha salama kwenye milima na mabonde hata nimefika leo hii

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa