Ingia / Jisajili

Nimekuchagua Wewe No. 2

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Ndoa

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 3,353 | Umetazamwa mara 8,387

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Nimekuchagua wewe, nimekuchagua wewe, katika tabu na raha uwe wangu wa maisha (x2). Sijaona mwingine, mzuri kama wewe, ndiyo maana nimekuchagua katika taabu na raha, mpaka kifo kitutenganishe (x2)

Mashairi:

1. Tutunze kiapo chetu, tutunze nadhiri zetu, tudumu katika pendo (kwani) ndiyo chimbuko la pendo, maisha tunayoanza upendo uyatawale, wito tuliochagua uendelee daima, tuishi kwa upendo, tuishi kwa upendo.

2. Sakramenti ya ndoa ituunganishe, sakramenti ya ndoa ituimarishe, sakramentui ya ndoa ichochee upendo wetu, sakramenti ya ndoa itupe furaha na amani.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa