Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,451 | Umetazamwa mara 5,842
Download Nota Download Midi
Kiitikio:
Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi yeyote anayevutiwa navyo hana hekima (x2)
Mashairi:
1. Usijionyeshe kuwa wewe u-hodari, hodari wa kunywa pombe, kwa maana pombe hiyo imeangamiza, imeangamiza wengi
2.Pombe ni kama uhai ukinywa kwa kiasi, pombe imewekwa ili itufurahishe itufurahishe nafsi zetu
3. Kunywa pombe kwa wakati tena kwa kiasi, pombe inaleta shangwe moyoni na furaha moyoni.
4. Kunywa pombe kupita kiasi kunasababisha kichwa kuuma, kunasababisha uchungu na fedheha.