Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,165 | Umetazamwa mara 6,100
Download Nota Download MidiKiitikio:
Mtumaini Mungu wako kwa moyo wako wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe, mtangulize Mungu wako katika kila jambo naye atazinyoosha njia zako zote.
Mashairi:
1. Mche Mungu wako, mche kila wakati, usijione mwenye hekima kuliko Mungu wako.
2. Mche Mungu wako ujiepushe na dhambi, usipomcha Mwenyezi Mungu utaangukia dhambini.
3. Kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo chanzo cha hekima, kumcha Mungu, kumcha Mungu chanzo cha maarifa.
4.Anayemtumaini Mwenyezi Mungu, hatatikisika kama mlima Sayuni.