Ingia / Jisajili

Njoni Tusemezane Asema Bwana

Mtunzi: Stanslaus Butungo
> Mfahamu Zaidi Stanslaus Butungo
> Tazama Nyimbo nyingine za Stanslaus Butungo

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Stanslaus Butungo

Umepakuliwa mara 1,442 | Umetazamwa mara 4,937

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Isaya 1:15-20, 26

Haya NJoni Tusemezane, haya njoni tusemezane, asema Bwana Mungu. Dhambi zenu japokuwa nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera zitakuwa kama sufu.

1. Huo wingi wa sadaka mnazonitolea una faida gani? Msilete tena mbele yenu matoleo ya ubatili siyapendi maovu yenu na mutano ya ibada

2. Jiosheni jitakaseni ondoeni uovu wa matendo yenu, acheni kutenda mabaya, jifunzeni kutenda mema, takeni hukumu kwa haki msaidieni aliyeonewa, mpatieni yatima haki yake msaidieni mjane.

3. Bali mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga. Ole wenu taifa lenye dhambi, miji yenu imeteketezwa kwa moto, wageni wamekula nchi yenu mbele ya macho yenu

4. Nanyi mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi. Nami nitawarejeza kwenu waamuzi wenu kama hapo mwanzo baada ya hayo mtakuwa mji mtakatifu mji wa amani.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa