Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 2,295 | Umetazamwa mara 7,285
Download Nota Download MidiKiitikio:
Kristo paska wetu amekwishakutolewa, amekwishakutolewa kuwa sadaka. basi na tuifanye karamu katika bwana tuile karamuye na tuimbe aleluya (x2)
Mashairi:
1. Kwa kujitoa kwake sadaka ya paska, tumetakaswa dhambi na kufanywa wateule, tumesafishwa mioyo kwa damu yake azizi, tukafanyiwa karamu ili sote tushiriki
2. Kifo chake Kristo kimetupatanisha, kimetupatanisha sisi na baba wa mbinguni, kimetuondolea dhambi ya asili na kutufanya tuwe wateule hata tushiriki meza yake.