Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 9,229 | Umetazamwa mara 23,516
Download Nota Download MidiKiitikio:
Sala yangu na ipae mbele yako Bwana (Ee Bwana) kama moshi wa ubani altareni (x 2). Na ipae, na ipae kama moshi wa ubani na kuinuliwa kwa mikono yangu, iwe kama sadaka ya jioni.
Mashairi:
1. Tunakusihi Ee Bwana uipokee sala yetu, ipae mbele yako kama moshi wa ubani, iwe kama sadaka ya mtumishi wako Abeli.
2. Hata matoleo yetu, kazi za mikono yetu, twayaleta mbele zako kwa unyenyekevu mkubwa, twakusihi Ee Bwana uyatakase, uyapokee kama shukrani yetu.
3. Vipaji hivi tunavyokutolea, vikupendeze, vikupendeze, vipae mbele zako kama moshi wa ubani, viwe kama sadaka ya jioni.