Ingia / Jisajili

Piga Hatua

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 357 | Umetazamwa mara 2,009

Download Nota
Maneno ya wimbo

Kushoto geuka, kulia geuka nyumba geuka, mbele geuka mguu sawa safari ianze tembea

  • Kiitikio:
  • Piga hatua, hatua piga hatua x2.  hatua moja kwenda kwa Yesu hatua moja kwenda kwa Yesu hatua moja  usirudi nyuma x2 mwendee Yesu ni jibu mwendee Yesu nijibu mwendee Yesu ni jibu x2

  • 1.Unapokuwa umeelemewa na mizigo mizito nenda nenda nenda wewe nenda, nenda kwa Yesu ndugu atakupumzisha.
  • 2.Magonjwa na vifo vikikusonga usikate, tamaa wewe nenda nenda kwa Yesu ndugu atakupumzisha.
  • 3.Na nguvu za giza zikikusonga usimwache Yesu ndugu mshikilie, tena mng'ang'anie ndoa yako ikikosa amani tulia usiende kwa waganga nenda kwa Yesu atakupumzisha.


  • Hitimisho:
  • (Ujue Yesu anakupenda) ae ae piga hatua (usijitenge naye hajakuacha) ae ae piga hatua (mkabidhi njia zako naye atafanya) ae ae piga hatua piga hatua kwenda kwa Yesu (mpe nafasi) atawale maisha yako, mwendee Yesu piga hatua.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa