Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 413 | Umetazamwa mara 2,046
Download NotaUtangulizi:
Ee Mungu uliyembingu ninakuita, Ee Mungu uliyembingu ninakuita, mfalme Sulemani alipokujengea hekalu Bwana alikunjua mikono, kukuelekea uliko juu mbinguni akisema ee Mungu ee Mungu wangu, mtu akiacha njia zako ukamghadhibikia, akiirudia nafsi nafsi nafsi yake akilikabiri hekalu hakalu nilikokujengea usikie huko mbinguni ukaitetee haki yake.
Kiitikio:
(nipe tena nafasi nyingine nipe tena Bwana Wangu nipe tena nafasi nyingine nikutumikie wewe x2)
Beti:
1.Uliniponipa kipaji, cha kukuimbia Mungu wangu kiburi kilinijaa majivuno na nyuma nikageuka nikakusahau hata uliponiadhibu, tazama narudi leo.
2.Niliteseka Mungu wangu, sipati mtoto miaka mingi kilio changu Bwana ulikisikia na mimba nikachukua Bwana nikaitoa kwa sababu ya anasa, najuta sina mtoto.
3.Uliniumba napendeza, Bwana ukanipa sura nzuri vilema niliwaona hawafai Bwana niliwatukana na leo nimepata ajali mbaya ya gari sina miguu wala mikono.
4.Uliponipa ajira, nilijua kuwa nimefika wasio na kazi niliwadharau niliona hawafai matusi niliwatukana kazini nimefukuzwa nimekuwa omba omba.