Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 1,108 | Umetazamwa mara 2,995
Download NotaSadaka yangu Bwana naileta Kwa moyo radhi na omba upokee x2 /(Mazao ya shambani ) pokea (fedha mifukoni) pokea (na mifugo yetu) pokea (nazo nia zetu) pokea pokea vyote ni mali yako./x2
1.Sadaka yangu haina kinyongo, nimeipata kwa juhudi zangu mwenyewe ninakusihi pokea pokea.
2.Bwana sileti ili nitazamwe, bali natoa toka ndani ya moyo wangu ninakusihi pokea pokea.
3.Hiki kidogo nilichoandaa, nimekipata Bwana wangu kwa wiki nzima ninakusihi pokea pokea.