Ingia / Jisajili

Sala Ya Mnyenyekevu

Mtunzi: John Mlewa
> Mfahamu Zaidi John Mlewa
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mlewa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Zaburi

Umepakiwa na: John Mlewa

Umepakuliwa mara 49 | Umetazamwa mara 72

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
||: Sala yake mtu mnyenyekevu, hupenya mawingu wala haitatulia, hata itakapowasili kwa Mungu:|| 1. Wala haitaondoka hata Aliye juu atakapoiangalia, akaamua kwa adili, akatekeleza hukumu. 2. Bwana hatomkubali yeyote juu ya maskini, naye ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa. 3. Bwana hatoyadharau kamwe malalamiko ya yatima, wala ya mjane amwelezapo habari zake. 4. Malalamiko yake aliyeonewa yatapata kukubaliwa, na dua yake itafika hima mbinguni, na dua yake itafika mbinguni

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa