Maneno ya wimbo
SASA NDIO WAKATI
1. Sasa ndio wakati wa kutoa sadaka,
kila mtu aanze kujifikiria.
Wiki nzima Bwana Mungu alikulinda vema,
sasa nawe ndugu yangu ujifikirie.
Kitikio
Toa ndugu, toa ndugu, ulicho nacho wewe.
Toa ndugu, toa ndugu, mpe Bwana sadaka.
Bwana anakuona mpaka moyoni mwako,
mpelekee Bwana mapato ya wiki.
2. Kumbuka jinsi Yesu alivyojitolea
pale msalabani kwa ajili yetu.
Tolea moyo wako, pia matendo yako
Naye Bwana Mungu akubarikie.
3. Mtolee Bwana sadaka ya mkate
na divai, atawabariki.
Baraka zake Mungu, za Baba na za Mwana,
Za Roho Mtakatifu, zikae nanyi nyote.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu