Ingia / Jisajili

Tujongee Meza Yake Bwana

Mtunzi: Dr. Nicholas Azza
> Mfahamu Zaidi Dr. Nicholas Azza
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Nicholas Azza

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Nicholas Azza

Umepakuliwa mara 177 | Umetazamwa mara 490

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
TOJONGEE MEZA YAKE BWANA 1. Tujongee meza yake Bwana, karibu kwenye karamu ya Bwana Yesu Kristo. Twende sote, anatuita! Kitikio Aulaye mwili wangu, na kuinywa damu yangu, yeye hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 2. Chakula ambacho Bwana ametuandalia ni mwili na damu yake, chakula cha uzima. 3. Kila wakati tunakula mkate na kunywa divai tunatangaza kifo chake na kukiri ufufuko wake. 4. Ninyi nyote mlio na njaa, ninyi nyote wenye kiu njooni mbele ya altareni naye atawashibisha.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa