Ingia / Jisajili

Yesu Anatuagiza Kuadhimisha Ekaristi

Mtunzi: Dr. Nicholas Azza
> Mfahamu Zaidi Dr. Nicholas Azza
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Nicholas Azza

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Nicholas Azza

Umepakuliwa mara 34 | Umetazamwa mara 55

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
YESU ANATUAGIZA KUADHIMISHA EKARISTI 1. Yesu anatuagiza kuadhimisha Ekaristi (Takatifu) kuutwaa mkate na kula, na kunywa divai. Tunapaswa kufanya hivyo kwa ukumbusho wake (Yesu) na kutangaza kifo chake hadi atakapokuja Enyi nyote (waumini) watu wa Mungu (njoo karibu), tunaitwa kwenye karamu ya Bwana Yesu Kristo. Tukusanyike (sisi sote) mezani pa Bwana (meza yake), tule chakula cha mbinguni alichotuandalia. 2. Katika Ekaristi Yesu anatupa (chakula) chakula kinachorutubisha miili yetu. Chakula anachotupatia (kwa upendo) pia ni kizuri kwa lishe yetu ya kiroho. Enyi nyote (ndugu zangu) watu wa Mungu (wakristo), Njooni, twende kwenye karamu ya Bwana Yesu Kristo. Tukusanyike (njooni ndugu) mezani pa Bwana (meza yake), tunywe kinywaji cha kiroho alichotuandalia. 3. Ekaristi ni sakramenti wa upendo wake (Yesu) ni ukumbusho wa dhabihu wa Kristo msalabani. Ekaristi hutuleta karibu na eye (Yesu), na inatuwezesha sisi wakristo kupendana. Enyi nyote (waumini) watu wa Mungu (njoo karibu), tunaitwa kwenye karamu ya Bwana Yesu Kristo. Tukusanyike (sisi sote) mezani pa Bwana (meza yake), tule chakula cha mbinguni alichotuandalia. 4. Ekaristi ni sakramenti ambayo ni muhimu (zaidi), ni chanzo na kilele cha maisha ya kikristo. Ekaristi ni mkate wa malaika wa mbinguni (huko juu), na ni zawadi na utukufu wa ukuhani. Enyi nyote (ndugu zangu) watu wa Mungu (wakristo), Njooni, twende kwenye karamu ya Bwana Yesu Kristo. Tukusanyike (njooni ndugu) mezani pa Bwana (meza yake), tunywe kinywaji cha kiroho alichotuandalia.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa