Ingia / Jisajili

Tembea Nami

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 1,458 | Umetazamwa mara 4,840

Download Nota
Maneno ya wimbo

Ee Mungu Mungu wangu uketiye huo juu mbinguni unasikia maombi yetu huko mbinguni unakotamalaki Bwana, Upewe sifa. Nilipokuwa hoi kitandani na matumaini yalipotea, ndipo nikafumba macho nikijua yametimia lakini Bwana ukaniponya, Upewe sifa.

Chorus

Ee Mungu pokea sifa na enzi pokea utukufu pokea Heshima na Shukrani za Moyo wangu. x2

  • Mashairi
    • 1.Nilipopatwa na ajali mbaya gari lilipopinuka nilijua yametimia lakini nikatoka mzima Bwana ukaniokoa Upewe Upewe upewe sifa.
    • 2.Maumivu ya kuonewa mimi machozi jasho na damu ni nafuu ya maisha yangu lakini Bwana wanipa amani moyoni na furaha Upewe upewe upewe sifa.
    • 3.Dhiki zote za maisha zangu njaa magonjwa msiba ukiwa vyote ni vyangu, machozi ndiyo faraja yangu Bwana ninakulilia sauti yangu sikia unikumbuke.

    • Hitimisho
    • (Ee Bwana niinue) niinue niinue Bwana (niinue) niinue niinue BWana (nishike mkono) niinue niinue Bwana (tembea nami Bwana) niinue niinue Bwana (Wewe ni Baba wa wajane) niinue niinue Bwana (Wewe ni Baba wa yatima) niinue niinue Bwana (Katika unyonge wangu) Tembea nami mwokozi (Katika shida na raha) tembea nami Mwokozi (Kamwe usiniache nyuma) tembea nami mwokozi (tembea) TEMBEA NAMI MWOKOZI.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa