Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 4,210 | Umetazamwa mara 9,705
Download Nota Download MidiHekalu lako limejaa harufu nzuri, harufu ya kuvutia ya manukato, manukato ya ubani na uvumba, hekalu lako limejaa harufu nzuri.
1. Haruni asubuhi na jioni alifukiza, hekalu lako limejaa harufu nzuri
Alifukiza manukato madhabahuni pako, hekalu lako limejaa harufu nzuri
2. Twaomba ibada yetu, twakusihi sala zetu, hekalu lako limejaa harufu nzuri
Zipae mbele yako kama moshi huu mzuri wa uvumba, hekalu lako limejaa harufu nzuri
3. Utubariki, ututakase, utuneemeshe, hekalu lako limejaa harufu nzuri
Ubani ishara ya uchaji heshima taadhima yetu, hekalu lako limejaa harufu nzuri
4. Uvumba zawadi ya unyenyekevu na kupondeka kwetu, hekalu lako limejaa harufu nzuri
Uvumba ni zawadi ya ukarimu wetu, hekalu lako limejaa harufu nzuri