Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: MICHAEL CHAINA
Umepakuliwa mara 3,071 | Umetazamwa mara 5,582
Download NotaSHAIRI
1.Uliumbwa kwa makusudi mazuri ya kupendeza maisha ya mawasiliano yawe rahisi kusudi binadamu pamoja tuutiishe ulimwengu tuliiombiwa na Mungu wetu na kisha wote tukatawale siku ya mwishi mbinguni tulikooandaliwa milele juu
2.Ulitumika vibaya bustanini kudanganyana Adamu na Hawa wakaanguka kwenye dhambi, ukatumika vizuri pale msalabani kupokea mapenzi ya Mungu kuyatimiza na kutuombea Msamaha kwa Mungu Baba ulimi ukaleta amani upatanisho
3.Kumbe ni uchaguzi wangu mwenyewe nitumiaje ulimi alionipa Mungu iwe faida,ulimi wangu uwe sababu ya wokovu, wokuvu wangu na wa wenzangu kwenda kwa Mungu kama nikitumia vibaya ulimi wangu heri ugandamane na kaa kaa la kinywa changu
KIITIKIO;
Ni mdogo kinywani mwangu mkubwa moyoni,ukitunza/zwa huleta amani faraja na tiba ukiachwa huzaa magomvi simanzi mauti ulimi wangu
N.B HII NI ORIGINAL COPY KUTOKA KWA MTUNZI NA WIMBO HUU UMEREKODIWA NA KWAYA YA MT.JEROME CHUO KIKUU IRINGA(IRINGA UNIVERSITY/TUMAINI)