Mtunzi: Peter Makolo
> Mfahamu Zaidi Peter Makolo
> Tazama Nyimbo nyingine za Peter Makolo
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Peter Makolo
Umepakuliwa mara 1,589 | Umetazamwa mara 4,388
Download Nota Download MidiYATUPASA KUMSHUKURU MUNGU Na: Peter Makolo
Kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa (January 29, 2013) Goteborg, SWEDEN
Nashuhudia waziwazi ni mwema sana
Jinsi anavyo tujali jinsi anavyotupenda
Anatupa na uzima pia anatuongoza
Hatuna cha kumlipa (Bwana wetu)
Kwa upendo wake,
{Yatupasa kumshukuru Mungu
Siku za maisha yetu yetu yote.} x2
Nashuhudia waziwazi ni mwema sana
Katutunza mpaka sasa ona tunavyopendeza
Ametupa familia nzuri na za kupendeza
Hatuna cha kumlipa (Bwana wetu)
Kwa upendo wake,
{Yatupasa kumshukuru Mungu
Siku za maisha yetu yetu yote.} x2
Nashuhudia waziwazi ni mwema sana
Anatupa mahitaji ya muhimu siku zote
Yupo nasi tutokapo yupo nasi turudipo
Hatuna cha kumlipa (Bwana wetu)
Kwa upendo wake,
{Yatupasa kumshukuru Mungu
Siku za maisha yetu yetu yote.} x2
Nashuhudia waziwazi ni mwema sana
Ametupa maarifa ya kupambanua mambo
Katujaza na Hekima tuweze kuelewana
Hatuna cha kumlipa (Bwana wetu)
Kwa upendo wake,
{Yatupasa kumshukuru Mungu
Siku za maisha yetu yetu yote.} x2
Nashudia waziwazi ni mwema sana
Tumrudishie nini kwa Upendo wake kwetu
Kinacholingana na fadhili zake kwetu sisi
Hatuna cha kumlipa (Bwana wetu)
Kwa upendo wake,
{Yatupasa kumshukuru Mungu
Siku za maisha yetu yetu yote.} x2