Mtunzi: Fred B. Kituyi
> Tazama Nyimbo nyingine za Fred B. Kituyi
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: FRED KITUYI
Umepakuliwa mara 1,714 | Umetazamwa mara 4,855
Download Nota Download MidiKiitikio:
Bwana unifanye chombo cha amani,
nikaeneze kote kote ulimwenguni, tukaishi kwa amani. x2
(Palipo chuki nilete pendo, penye ugomvi nilete patano, (Ee!)
Tupendane, tupendane kama vile Yesu anavyotupenda. x2)
1. Nikiwa nao upendo, nitaeneza amani:
(Sote tutaishi nayo furaha – furaha yake Mungu. x2)
2. Upendo hauna chuki, upendo hauna wivu:
(Upendo wa kweli hutoka kwake - Mwenyezi Mungu Baba. x2)
3. Upendo huvumilia, na hauoni mabaya:
(Ee Baba naomba nipe upendo - nipe nayo amani. x2)
4. Nikiwa nayo imani, ya kuhamisha milima:
(Nisipokuwa na ule upendo - mimi ni kitu bure. x2)