Ingia / Jisajili

Usitende Dhambi Tena

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 910 | Umetazamwa mara 4,455

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Nenda zako, nenda na tangu sasa usitende dhambi tena, na tangu usitende dhambi tena, usitende dhambi tena (x2)

Mashairi:

1. Maneno hayo aliyasema Yesu pale walimu wa sheria na mafarisayo walipomshitaki mwanamke mmoja kwa uzinzi, wakimjaribu Yesu, ili wapate sababu ya kumshitaki mwanamke yule.

2.Maneno hayo aliyosema Yesu ni fundisho kwetu sisi sote tusiwe na mioyo ya kuhukumu wengine, kwani sote tu wadhambi, tusihukumu, kwani sote tu wadhambi, tusiwe kama wale mafarisayo na walimu wa sheria.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa