Ingia / Jisajili

Utenzi & Sala Kwa Mungu Mwaminifu

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi | Tenzi za Kiswahili

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 1,127 | Umetazamwa mara 4,318

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

1. Fadhili za Bwana nitaziimba milele, kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote, nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wangu, maana nimesema fadhili zitajengwa milele katika mbingu nitauthibitisha uaminifu wako.

2. Nimefanya agano na mteule wangu, nimemwapia Daudi mtumishi wangu, wazao wako nitawafanya imara milele, nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.

3. Ee Bwana mbingu zitayasifu maajabu yako, uaminifu wako katika kusanyiko la Watakatifu, maana ni nani katika Mbingu wa kulinganishwa na wewe ni nani afafanaye na Bwana miongoni mwa malaika

4. Mungu huogopwa sana barazani pa Watakatifu, ni wa kuhofiwa kuliko wote wamzungukao, Bwana Mungu wa majeshi ni nani aliye hodari kama wewe uaminifu wako unakuzunguka


Maoni - Toa Maoni

Noel Jul 06, 2017
Tumsifumungu tuki imbatenzi o

Toa Maoni yako hapa