Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,464 | Umetazamwa mara 6,822
Download Nota Download MidiKiitikio:
Neno moja nimelitaka kwa bwana, nimelitaka kwa bwana, nalo ndilo nitakalolitafuta (x2). Nikae nyumbani mwa bwana, nikae nyumbani mwa bwana, nikae nyumbani mwa bwana milele; niutazame uzuri wake hekaluni mwake (x2)
Mashairi:
1. Mradi bwana atanisitiri bandani mwake, atanisitiri ile siku ya mabaya, atanisitiri katika sitara yake ya hema yake na kuniinua juu ya mwamba.
2. Basi kinywa changu kitainuka juu ya adui zangu wanaonizunguka, nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake, nitaimba, nitaimba, Naam; nitamhimidi bwana.